Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kamusoko nje, Chirwa ndani kikosi cha Yanga leo

Muktasari:

Kamusoko aliumia kwenye mchezo dhidi ya Njombe Mji lakini alifanya mazoezi hadi Jana Ijumaa lakini Daktari wa Yanga, Edward Bavu ameona ni vyema akapumzishwa.

Songea. Nahodha wa Yanga, Thaban Kamusoko ameondolewa kwenye kikosi cha Yanga kitakachocheza na Majimaji leo huku Mzambia, Obrey Chirwa akianza mechi yake ya kwanza msimu huu.
Kamusoko aliumia kwenye mchezo dhidi ya Njombe Mji lakini alifanya mazoezi hadi Jana Ijumaa lakini Daktari wa Yanga, Edward Bavu ameona ni vyema akapumzishwa.
Kwa upande wa Chirwa, ameingia kwenye kikosi cha kwanza leo baada ya kupata dakika chache kwenye mchezo uliopita.
Katika hatua nyingine, Geofrey Mwashiuya na Raphael Daudi wameingia kwenye kikosi cha kwanza kwa mara ya kwanza msimu huu.
Daudi aliingia akitokea benchi katika mechi mbili za mwanzo lakini leo ameanza badala ya Kamusoko.
Yanga itavaana na Majimaji leo saa 10 jioni na tayari mashabiki wameanza kuingia uwanjani.