Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kaimu Meneja Kwa Mkapa, wengine sita wasimamishwa kazi

Muktasari:

  • Baadhi ya wengine waliosimamishwa kazi ni aliyekuwa Mhandisi wa Umeme, Manyori Kapesa , aliyekuwa Afisa Tawala, Tuswege Nikupala. Aidha, rungu hilo limewapitia wafanyakazi wengine wa uwanja huo akiwemo, Gordon Mwangamilo, Gabriel Mwasele, Yanuaria Imboru na Dk Christina Luambano.

Waziri wa Sanaa, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Dk Pindi Chana amewasimamisha kazi watumishi saba wakipisha uchunguzi akiwemo Kaimu Meneja wa Uwanja wa Mkapa, Salum Mtumbuka baada ya tatizo la kukatika umeme uwanjani hapo kujirudia mara mbili tofauti wakati wa mechi ya Taifa Stars dhidi ya Uganda kufuzu Afcon Machi 28, 2023 na jana Aprili 30 mechi ya robo fainali Kombe la Shirikisho kati ya Yanga na Rivers United.

Baadhi ya wengine waliosimamishwa kazi ni aliyekuwa Mhandisi wa Umeme, Manyori Kapesa , aliyekuwa Afisa Tawala, Tuswege Nikupala. Aidha, rungu hilo limewapitia wafanyakazi wengine wa uwanja huo akiwemo, Gordon Mwangamilo, Gabriel Mwasele, Yanuaria Imboru na Dk Christina Luambano.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Saidi Yakubu amemteua Mlinde Mahona kuwa Kaimu Meneja wa Uwanja wa Mkapa kuanzia leo Mei Mosi, 2023.