Juma Abdul, Mbrazili Coutinho jukwaani

Muktasari:
Pia kiungo wao, Mbrazili Andrey Coutinho naye atakuwa mtazamaji jukwaani kutokana na maumivu ya goti mguu wa kulia. Daktari wa Yanga, Richard Yomba, amesema mbali ya Coutinho, hana majeruhi wa kutia wasiwasi.
YANGA itamkosa beki wake wa kulia, Juma Abdul mwenye kadi tatu za njano katika mechi ya kesho Jumapili dhidi ya Simba huku Katibu wao, Dk. Jonas Tiboroha akisema hawataingia kwenye mtego kwa kutumia mbinu ya kuchagua mechi kama walivyofanya watani wao Simba waliomchezesha Ibrahim Ajibu mechi na Prisons.
Pia kiungo wao, Mbrazili Andrey Coutinho naye atakuwa mtazamaji jukwaani kutokana na maumivu ya goti mguu wa kulia. Daktari wa Yanga, Richard Yomba, amesema mbali ya Coutinho, hana majeruhi wa kutia wasiwasi.
Yanga inajivunia uwepo wa wachezaji sita waliocheza Simba; Kelvin Yondani, Mrisho Ngassa, Mrundi Amissi Tambwe, Danny Mrwanda na makipa Ally Mustapha ‘Barthez’ na Deo Munishi ‘Dida’.
Miongoni mwa hao ni tegemeo kwenye kikosi cha kwanza na wanaijua vizuri Simba, hivyo itakuwa rahisi kwa Yanga kujua mbinu za Wekundu wa Msimbazi hao.
Mastraika kama, Mrwanda, Ngassa na Tambwe watakuwa msaada tosha kwa Yanga katika mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara. Mrwanda alisema: “Tutahakikisha tunaifunga Simba.”
Kikosi cha kuiua Simba; Barthez, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Yondani, Said Juma, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Tambwe, Ngassa na Mrwanda.