Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

JKT Queens kundi moja na Mamelodi

Klabu ya JKT Queens imepangwa kundi A katika michuano ya Ligi ya Mabingwa kwa Wanawake yatakayofanyika nchini Ivory Coast kuanzia Novemba 5 hadi 19 mwaka huu.

Katika kundi hilo atavaana na timu za Atletico FC ya Ivory Coast akiwa mwenyeji, Sporting Casablanca ya Morocco na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ambao walitwaa ubingwa wa michuano hiyo 2021.

JKT Queens ilipata nafasi hiyo baada ya kushinda ubingwa wa Ligi ya Wanawake nchini na ubingwa wa CECAFA.

JKT Queens Wametwaa Ubingwa huo baada ya Kuifunga CBE ya Ethiopia ambayo waliingia nao fainali, ambapo mechi hiyo ilichezwa Jinja Nchini Uganda.