Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jesca anaendelea alipoishia WBDL

Muktasari:

  • Ngisaise aliyechipukia katika kituo cha Ukonga Akademy, ligi ya mwaka jana aliibuka mfungaji bora akiwa na pointi 584, akifuatiwa na Elina Sinasega wa Twalipo Queens aliyefunga  pointi 353.

NYOTA wa JKT Stars, Jesca Ngisaise ameendelea kudhihirisha ubora wake wa kutupia, baada ya kufunga pointi 94 katika mechi mbili za Ligi ya kikapu Dar es Salaam kwa Wanawake (WBDL).  

Ngisaise aliyechipukia katika kituo cha Ukonga Akademy, ligi ya mwaka jana aliibuka mfungaji bora akiwa na pointi 584, akifuatiwa na Elina Sinasega wa Twalipo Queens aliyefunga  pointi 353.

Pia nyota huyo aliongoza kwa kufunga mitupo ya pointi tatu na kufikisha 59, akifuatiwa na Irene Gerwin wa DB Troncatti aliyefunga 38.

Katika mechi ya kwanza mwaka huu ya ushindi mnono wa pointi 64-46 dhidi ya DB Troncatti, iliyopigwa Viwanja vya Donbosco, Upanga, alifunga pointi 28, huku dhidi ya UDSM Queens walioshinda 145-28, alifunga pointi 66.

Alifuchua kinachombeba kwenye ufungaji ni mazoezi binafsi ya kufunga anayofanya kabla ya kuanza ya pamoja na timu.

“Kwa kweli kama unataka uwe mfungaji, unatakiwa  ujitoe,  ni pamoja na kupanga muda wako wa mazoezi, bila ya hivyo huwezi ukafanya vizuri,” alisema Jesca.