Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ishu ya Singida Big Stars, US Monastir usipime

KAMA ulidhani Singida Big Stars inatania basi sahau hilo unaambiwa, baada ya Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu, John Kadutu kuweka wazi wana malengo ya kuhakikisha kikosi hicho kinafanya vizuri ndani na nje ya mipaka ya nchi.

Kauli ya Kadutu inajiri baada ya timu hiyo kuingia mkataba wa ushirikiano wa masuala ya utawala, uendeshaji na ufundi na klabu ya US Monastir ya Tunisia ikiwa ni muda mchache tu tangu icheze na Yanga kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

“Hii ni fursa kubwa kwetu ya kuendelea kuitangaza timu yetu nje ya mipaka ya Tanzania, wakati tunaanza watu walituchukulia kawaida tu lakini mambo tunayoyafanya wanaanza kuamini hatutanii na tumedhamiria,” alisema.

Aidha Kadutu aliongeza kupitia timu hiyo watapata nafasi ya kuendelea kujifunza mambo mengi hasa ya jinsi ya kiuendeshaji na utawala bora kwenye klabu yao ambao utawasaidia kutimiza malengo yao ya muda mfupi na mrefu.

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Hans Van Der Pluijm alisema kupitia ushirikiano huo anaamini utakuwa na manufaa makubwa kwao hususan kwenye malengo yao waliyojiwekea ya kuleta ushindani kwenye soka nchini.

Pamoja na mambo mengine yaliyojadiliwa juzi baina ya viongozi wa timu zote mbili ila Singida BS imepata ofa maalumu ya kuweka kambi ya maandalizi ya msimu (Pre-Season) kwa msimu wa 2023/2024 nchini Tunisia kwa hisani ya Monastir.