Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Iringa kujenga uwanja wa gofu

IRINGA Pict

Muktasari:

  • Kwa miaka mingi Iringa imekuwa na uwanja mmoja wa gofu wa Mufindi uliojengwa na Kampuni ya kikoloni ya Brooke Bond uliopo katika mashamba ya chai na wazo hilo lilitolewa na wachezaji wakongwe wa mchezo huo kutoka mkoa huo, Edmund Mkwawa na Alfred Kinswaga waliofika katika Klabu ya Lugalo, jijini Dar es Salaam.

MKOA wa Iringa umeanza mkakati wa kujenga uwanja wa kisasa wa gofu utakaojulikana kama Mkwawa Golf Course ili kuendeleza mchezo huo mkoani huo na nchini kwa jumla.

Kwa miaka mingi Iringa imekuwa na uwanja mmoja wa gofu wa Mufindi uliojengwa na Kampuni ya kikoloni ya Brooke Bond uliopo katika mashamba ya chai na wazo hilo lilitolewa na wachezaji wakongwe wa mchezo huo kutoka mkoa huo, Edmund Mkwawa na Alfred Kinswaga waliofika katika Klabu ya Lugalo, jijini Dar es Salaam.

Nahodha wa gofu katika klabu ya Lugalo, Meja Japhet Masai, Mweka Hazina, Kapteni Mtuya na Mratibu wa Chama cha Gofu Tanzania, Johnson John ndio walioupokea ujumbe huo kutoka Iringa mwishoni mwa juma na kujadili na kushauriana namna bora ya kuutekeleza mpango huo.

“Ilikuwa ni faraja kwetu kuupokea ujumbe wa wanafamilia ya gofu kutoka Iringa na azma yao njema ya kutaka kujenga uwanja wa kisasa wa gofu mkoani humo. Tunamshukuru pia kiongozi wa msafara na mcheza gofu mkongwe, Edmund Mkwawa kwa kuja kwetu.

“Pia tunamshukuru bwana Alfred Kinswaga, mcheza gofu na mdau mkubwa wa maendeleo ya gofu nchini pamoja na wajumbe kutoka hamashauri ya Mji wa Iringa aliofuatana nao,” alisema Meja Masai.

Kwa mujibu Masai, Lugalo imekuwa ni klabu ya kuigwa kwa kuwa na mipango thabiti ya kuukuza mchezo huo kuanzia ngazi ya vijana, wanawake na wakongwe wa mchezo.

Alisema ujumbe huo pia unataka kujua namna bora ya kutunza na kuboresha viwanja vyote 18 vya gofu ikiwa ni pamoja na kuandaa mashindano yanayokidhi hadhi ya kitaifa na kimataifa.

Kuwepo kwa uwanja wa pili mkoani Iringa kutaongeza idadi ya viwanja vya gofu nchini na miaka ya nyuma kulikuwep na viwanja sita tu vya gofu nchi nzima na sasa kuna vingi vimejengwa vikiwamo vya Misenyi (Kagera), Kilombero (Morogoro), Kili Golf (Arusha) na  Sea Cliff (Zanzibar) na sasa unatarajiwa wa Mkwawa Golf course cha Iringa.