Ilanfya mambo freshi, mjipange

Muktasari:
- Ilanfya alisema licha ya kukaa nje alikuwa anafanya mazoezi na kufuatilia Ligi Kuu ili kujua kinachoendelea, na kilichomvutia zaidi ni kiwango walichokionyesha wazawa kama mshambuliaji wa Yanga Clement Mzize aliyemaliza na mabao 14 na asisti tano.
BAADA ya mshambuliaji wa JKT Tanzania, Charles Ilanfya kukaa nje kwa msimu mzima akiuguza jeraha la goti la kulia aliloumia kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Azam, amesema atarejea kivingine 2025/26.
Ilanfya alisema licha ya kukaa nje alikuwa anafanya mazoezi na kufuatilia Ligi Kuu ili kujua kinachoendelea, na kilichomvutia zaidi ni kiwango walichokionyesha wazawa kama mshambuliaji wa Yanga Clement Mzize aliyemaliza na mabao 14 na asisti tano.
“Wapo makipa ambao wamefanya kazi nzuri kama Yona Amos wa Pamba (clean sheets 11), Patrick Munthari wa Mashujaa (12) na Yakoub Ali wa JKT Tanzania (nane), huku Feisal Salum wa Azam akiwa na asisti 13, mabao manne, Nassor Saadun (mabao manane) wapo wengi na hao ni baadhi tu,” alisema.
“Kwa upande wa wageni ambao wamefanya vizuri kuonyesha uwezo binafsi ni Pacome Zouzoua mabao 12, asisti 10 na Maxi Nzengeli mabao sita na asisti 10. Hao jamaa wana vitu vya kipekee kiufundi hasa uamuzi wao wanapokuwa na mpira mguuni.”