Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Huko Championship ukizubaa tu umeachwa

CHAMPIONSHIP Pict

Muktasari:

  • Vinara wa Ligi hiyo, Geita Gold inayoongoza ikiwa na pointi 58 baada ya kuichapa B19 FC mabao 2-0, mechi iliyopita, leo itakuwa kwenye Uwanja wa Nyankumbu mjini, Geita kuikaribisha Mbuni ya jijini, Arusha iliyoichapa Stand United bao 1-0.

VITA ya kusaka tiketi ya kucheza Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao wa 2026-2027 inaendelea tena wikiendi hii kwa kushuhudia raundi ya 24 ya Ligi ya Championship ikishika kasi, huku ushindani ukiendelea kwa kila timu kujiwekea mazingira mazuri.

Vinara wa Ligi hiyo, Geita Gold inayoongoza ikiwa na pointi 58 baada ya kuichapa B19 FC mabao 2-0, mechi iliyopita, leo itakuwa kwenye Uwanja wa Nyankumbu mjini, Geita kuikaribisha Mbuni ya jijini, Arusha iliyoichapa Stand United bao 1-0.

Geita Gold ni vinara wa Ligi ya Championship kwa sasa ikiwa na pointi 55 baada ya kushinda mechi 18 ikitoka sare nne na kuchapwa moja, ikifunga mabao 46 na kuruhusu 13 ikipambana kurejea Ligi Kuu baada ya kushuka msimu wa 2023-2024.

CHAMP 01

Timu hiyo iliyoshuka daraja msimu wa 2023-2024, msimu wa 2024-2025, wa Championship ilimaliza nafasi ya nne na pointi 56 chini ya aliyekuwa Kocha Mkuu Mohamed Muya na kushindwa kurejea Ligi Kuu Bara baada ya kufeli mechi za play-off (mchujo).

Geita ilicheza mchujo ya kupanda Ligi Kuu Bara dhidi ya Stand United ‘Chama la Wana’ iliyomaliza nafasi ya tatu na pointi 61 na kushuhudiwa ikiondoshwa kwa jumla ya mabao 4-2, baada ya sare nyumbani ya 2-2, kisha kuchapwa ugenini 2-0.

Kwa upande wa Mbuni FC, msimu huu imekuwa haina mwenendo mzuri katika Ligi ya Championship ambapo kikosi hicho kutokea Arusha, kiko nafasi ya sita na pointi 41, baada ya kushinda mechi 13, sare mbili tu na kupoteza nane kati ya 23. Kagera Sugar inayoshika nafasi ya pili na pointi 55, baada ya kuifunga Hausung FC mabao 2-0 itaendelea kubakia ugenini ambapo itakuwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid - Arusha kucheza dhidi ya TMA FC iliyoichapa Gunners FC ya Dodoma 2-0.

CHAMP 02

Kagera iliyodumu katika Ligi Kuu Bara kwa miaka 20 tangu ilipoanza kushiriki 2005, ilishuka daraja msimu wa 2024-2025 baada ya kushinda mechi tano, sare nane na kupoteza 17, ikishika nafasi ya 15 kufuatia kukusanya pointi zake 23.

Timu hiyo inayonolewa na aliyekuwa nyota wa Simba, Yanga na timu ya Taifa Stars, Juma Kaseja aliyewahi kuitumikia pia Kagera akiwa mchezaji na kocha wa makipa ana kazi ya kukipambania kikosi hicho ili kirejee tena katika Ligi Kuu Bara.

Kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora, Mbeya Kwanza iliyopo nafasi ya tatu na pointi 51 baada ya kuifunga Songea United mabao 2-0 itacheza dhidi ya Hausung FC ya Njombe iliyotoka kuchapwa mechi ya mwisho na Kagera Sugar mabao 2-0.

CHAMP 03

Stand United ‘Chama la Wana’ iliyotoka kuchapwa na Mbuni FC bao 1-0 mechi yao iliyopita itakuwa kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga kucheza dhidi ya maafande wa Transit Camp walioichapa African Sports kutoka Tanga mabao 4-2.

Msimu uliopita Stand ilimaliza ikiwa nafasi ya tatu na pointi 61 ambapo ilicheza mchujo wa kupanda Ligi Kuu Bara ikianza kwa kuiondosha Geita Gold iliyomaliza ya nne na pointi 56 katika Ligi ya Championship kwa jumla ya mabao 4-2.

Baada ya Stand kuitoa Geita Gold ikacheza mchujo mwingine na Fountain Gate iliyotolewa pia hatua hiyo na maafande wa Tanzania Prisons kwa jumla ya mabao 4-2, ambapo kikosi hicho kilikwama kupanda baada ya kufungwa jumla ya mabao 5-1.

CHAMP 04

Msimu huu wa 2025-2026, Stand inashika nafasi ya 13 na pointi 20, baada ya kushinda mechi saba, sare mbili na kupoteza 14, kati ya 23, iliyocheza, huku safu yake ya ushambuliaji ikifunga mabao 19 na kuruhusu nyavu zake kutikiswa mara 33.

Mechi ya mwisho leo Jumamosi itapigwa kwenye Uwanja wa Ushirika mjini, Moshi ambapo maafande wa Polisi Tanzania baada ya kuichapa Barberian FC mabao 3-1 itaikaribisha Songea United, yenye kumbukumbu ya kuchapwa na Mbeya Kwanza mabao 2-0.

Polisi msimu uliopita wa 2024-2025, haukuwa mzuri sana baada ya kumaliza nafasi ya 10 katika Ligi ya Championship na pointi 33 ikishinda mechi nane, sare tisa na kupoteza 13, ambapo safu ya ushambuliaji ilifunga mabao 44 na kuruhusu 33.

CHAMP 05

Kikosi hicho kinachopambana ili kurejea Ligi Kuu Bara baada ya kushuka daraja msimu wa 2022-2023, kilipomaliza nafasi ya 15 na pointi 25, msimu huu kiko nafasi ya nne na pointi 48, kikishinda mechi 14, kikitoka sare sita na kupoteza tatu.

Raundi ya 24 itaendelea kesho Jumapili kwa mechi tatu kupigwa ambapo African Sports iliyochapwa mabao 4-2 na Transit Camp itakuwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga kuikaribisha KenGold iliyotoka sare ya bao 1-1 na Bigman FC.

Kwenye Uwanja wa Ilulu, Lindi, wenyeji, Bigman FC itaikaribisha B19 FC, huku Barberian FC inayoburuza mkiani mwa msimamo ikiwa nafasi ya 16 na pointi 10, itacheza dhidi ya Gunners FC ya Dodoma, iliyotoka kuchapwa mabao 2-0 mbele ya TMA FC.

Kocha Mkuu wa Geita Gold, Zubery Katwila amesema ushindani umekuwa ni mkubwa kwa sasa kutokana na mahitaji ya kila timu hasa kwa mechi hizi za mwishoni ingawa malengo yao ni kuhakikisha kikosi hicho kinarejea Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao.

“Presha ni kubwa sana kwa sababu timu yoyote unayokutana nayo tayari ina malengo yake iliyojiwekea, jambo linaloongeza ushindani zaidi, tutaendelea kucheza pia kwa tahadhari ili tuhakikishe tunatimiza kile tulichokusudia,” amesema Katwila.