Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hersi: Bado ahadi moja Yanga

AHADI pict

Muktasari:

  • Akizungumza na mashabiki wa Yanga makao makuu ya klabu hiyo, amesema waliahidi kuwa na mabadiliko ya uendeshaji wa klabu ambayo amethibitisha kuwa hivi karibuni wanachama watajua thamani ya klabu hiyo.

RAIS wa Yanga, Hersi Said amesema anadaiwa ahadi moja kati ya tano walizoahidi walipopewa ridhaa ya kuongoza klabu hiyo.

Akizungumza na mashabiki wa Yanga makao makuu ya klabu hiyo, amesema waliahidi kuwa na mabadiliko ya uendeshaji wa klabu ambayo amethibitisha kuwa hivi karibuni wanachama watajua thamani ya klabu hiyo.

Pia ametaja ahadi ya pili kuwa ni kujenga kikosi imara ambacho  wamefanikiwa kwa asilimia kubwa na ndicho kilichowapa mafanikio kwa misimu minne mfululizo.

Tatu amesema kuwa wao kama viongozi waliahidi kuhakikisha Yanga inajisimamia suala ambalo wamefanikiwa kwa kutafuta wadhamini ambao kwa asilimia kubwa wameifikisha klabu hiyo katika mafanikio.

Ahadi ya tano na ya mwisho, Hersi amesema wamekwama kujenga uwanja ambao ameahidi kuwa upo kwenye mchakato baada Serikali kuwapa ridhaa ya kujenga makao makuu ya klabu.

“Tulitakiwa kupata eneo kubwa ambalo lingefaa kujenga uwanja wa kisasa na miradi mingine mingi, tunaishukuru Serikali ya awamu ya sita kutupa ridhaa ya kujenga uwanja,” amesema.