Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hatima ya Tanzania kuandaa Afcon leo

UAMUZI mkubwa na muhimu unaohusu hatima ya Tanzania na mataifa mengine mawili kutoka Afrika Mashariki kuandaa michuano ya Kombe la Afrika 2027 utafahamika leo Jumatano.

Tanzania imeungana na Kenya na Uganda kuwasilisha ombi walilolibatiza jina la ‘Pamoja Bid’ wakiwa na matumaini kwa mara ya kwanza ukanda wa Afrika Mashariki utaandaa michuano hiyo mikubwa ya soka.

Kwa Kenya itakuwa ni mara ya pili inajaribu kuomba kuwa mwenyeji baada ya ombi la kwanza 1996 kukubaliwa, lakini baadaye wakapokonywa na kuhamishiwa Afrika Kusini.

Mwaka 2017, Kenya waliomba tena kuwa mwenyeji lakini safari hii michuano ya Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa ndani (CHAN) ombi ambalo pia lilikubaliwa ila kwa mara nyingine tena wakapokonywa na michuano hiyo kuhamishiwa Rwanda.

Wiki iliyopita, Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Damas Ndumbalo aliondoka nchini kwenda Muisri kwa ajili ya kupigia chapuo jambo hilo ambalo linaungwa mkono kwa karibu kabisa na Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na marais Yoweri Museveni wa Uganda na Dk William Ruto (Kenya).

Hatima ya Pamoja Bid itafahamika leo pale wajumbe wa Kamati ya Utendaji CAF itakapokutana jijini Cairo, Misri kutangaza nchi wenyeji wa michuano ya Kombe la Afrika 2027.

CAF pia inatarajiwa kutaja taifa litakaloandaa Kombe la Mataifa ya Afrika 2025 kutokana na Guinea kupoteza sifa Oktoba mwaka jana baada ya kubainika taifa hilo lililo Magharibi mwa Afrika lilikuwa nyuma ya wakati kwenye maandalizi ya michuano hiyo itakayoshirikisha mataifa 24.

Mataifa yanayowania kuwa mwenyeji wa Afcon 2025 ni Algeria, Morocco, Zambia na muunganiko wa Benin na Nigeria, wakati Pamoja Bid inatunishana misuli kuwa mwenyeji Afcon 2027 dhidi ya Algeria, Botswana na Misri.

Moja ya vigezo vya CAF kwa nchi kuwa mwenyeji wa Afcon ni uwepo wa viwanja sita ambapo viwili viwe na uwezo wa kuchukua kila kimoja watu 40,000 na vingine viwili kila kimoja kiikichukua watu 20,000 na pia viwanja viwili kila moja kikiwa na uwezo wa kuchukua watu 15,000.

Hii ni kumaanisha kwa nchi tatu za Afrika Mashariki, kila moja lazima iwe na viwanja viwili vyenye hadhi ya kimataifa ingawa kwa Tanzania hilo halina shida kutokana na uwepo wa Uwanja wa Mkapa, Uwanja wa Amaan Zanzibar, Uwanja wa Azam Complex na marekebisho kidogo kwenye viwanja vya CCM Kirumba Mwanza, Sheikh Amri Abeid Arusha na vingine vingi.