Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Guu la beki wa Mtibwa noma sana

Muktasari:

Mchezaji anayemfuata kwa ukaribu wa ukubwa wa mguu ni Joseph Owino raia wa Uganda anayecheza Simba ambaye anavaa namba 11.5 au 12 na Oscar Joshua wa Yanga anayevaa namba 10.

MGUU wa beki wa kati wa Mtibwa Sugar, Salim Mbonde ni kiboko aisee, kwani amewapiga bao wachezaji wote wa Simba na Yanga na kuwa kinara wa kuvaa kiatu chenye saizi kubwa yaani namba 13, ambayo hata kupatikana madukani ni shida.

Mchezaji anayemfuata kwa ukaribu wa ukubwa wa mguu ni Joseph Owino raia wa Uganda anayecheza Simba ambaye anavaa namba 11.5 au 12 na Oscar Joshua wa Yanga anayevaa namba 10.

Mbonde aliliambia Mwanaspoti: “Navaa kiatu namba 13 ambayo imekuwa inanipa wakati mgumu kupata saizi yangu. Vinapokuja viatu vya timu, mimi huwa nakosa lakini bosi wetu Bayser (Jamal, Mratibu wa Mtibwa), ndiye anayeniletea vyangu  anajua anapovipata.”

Kocha msaidizi wa Mtibwa, Zubeir Katwila alisema: “Mbonde anavaa kitu namba 13 na hivi karibuni tulipokuwa kwenye Kombe la Mapinduzi tulizunguka maduka yote ya Zanzibar hatukupata namba yake, ikabidi Bayser aje navyo kutoka Dar es Salaam.”

“Na mchezaji anayevaa kiatu chenye saizi ndogo katika kikosi chetu ni Vincent Barnabas. Yeye anavaa namba sita,” alisema Katwila mchezaji wa zamani wa kikosi hicho.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amethibitisha kuwa, katika kikosi cha Yanga, Oscar ndiye anayevaa kiatu kikubwa namba 10, wakati Mnyarwanda Haruna Niyonzima na Juma Abdul ndiyo wanaovaa saizi ndogo ambayo ni namba 6.5.

Naye meneja wa Simba, Nico Nyagawa ameweka wazi kuwa, Owino ndiye anayevaa kiatu kikubwa kuliko mchezaji mwingine ambacho ni namba 12, wakati Ibrahim Ajib na Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ ndiyo wanavaa saizi ndogo ambayo ni namba sita.