Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gomez aja kivingine Fountain Gate

Muktasari:

  • Nyota huyo mwenye mabao sita Ligi Kuu Bara sawa na Clement Mzize wa Yanga, akipitwa na Elvis Rupia wa Singida Black Stars aliyefunga manane na Jean Charles Ahoua wa Simba mwenye saba, amecheza michezo 10  kati ya 16 ya kikosi hicho. Lakini sasa amerejea kuitumikia timu hiyo akisema anajiandaa vya kutosha.

MSHAMBULIAJI nyota na kinara wa mabao wa Fountain Gate (FOG), Selemani Mwalimu ‘Gomez’ ameanza mazoezi baada ya kuwa nje tangu Desemba 29, mwaka jana kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya nyama za paja akikosa michezo sita ya Ligi Kuu Bara.

Nyota huyo mwenye mabao sita Ligi Kuu Bara sawa na Clement Mzize wa Yanga, akipitwa na Elvis Rupia wa Singida Black Stars aliyefunga manane na Jean Charles Ahoua wa Simba mwenye saba, amecheza michezo 10  kati ya 16 ya kikosi hicho. Lakini sasa amerejea kuitumikia timu hiyo akisema anajiandaa vya kutosha.

“Kwa sasa naendelea vizuri na matumaini yangu ni kuona narejea katika ubora wangu ambao mashabiki wameuzoea tangu mwanzoni mwa msimu. Nina kazi kubwa ya kufanya kwa sababu nimekaa nje muda mrefu na tupo na benchi jipya la ufundi,” alisema Gomez aliyekuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Zanzibar msimu uliopita akiwa KVZ.

Akizungumzia benchi jipya la timu hiyo chini ya Mkenya Roberto Matano, Mwalimu alisema licha ya uhodari wa kufunga ana kazi ya kumshawishi kocha huyo kwa sababu ni mgeni, huku ushindani ukiwa pia mkubwa miongoni mwao.

“Wakati wa Mohamed Muya sio kwamba nilikuwa nacheza kwa sababu tumezoeana isipokuwa ni jitihada nilizoonyesha. Amekuja Matano naye atahitaji kuona nikionyesha kiwango bora ili anipe nafasi, nimepania makubwa mzunguko wa pili.”

Mara ya mwisho kwa mchezaji huyo kufunga bao katika Ligi Kuu Bara ilikuwa kwenye ushindi wa kikosi hicho wa mabao 3-1 dhidi ya KMC, Oktoba 21, mwaka jana na sasa akifikisha siku 101 ambazo ni sawa na miezi mitatu na siku tisa bila ya kuona nyavu za wapinzani. Fountain Gate ipo katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi.