Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gomes: Kichapo kinawahusu

KOCHA wa Simba, Didier Gomes Da Rosa amewapa sharti wachezaji wake la kupata ushindi katika mechi zote walizobakiza msimu huu ili kuwafuta mashabiki machozi ya kutolewa katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na timu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

Gomes aliiambia Mwanaspoti kuwa kutokuwapo katika Ligi ya Mabingwa Afrika, kunawapa fursa nzuri ya kutetea taji la Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la Azam lakini pamoja na hilo, anataka kuona wanathibitisha ubora wao kwa kuibuka na ushindi katika michezo yao yote waliyobakiza.

“Kwa sasa hatumo katika mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika na akili yetu tunairudisha katikia mashindano ya ndani. Tuko vizuri katika Ligi Kuu ambako tunahitaji kupata ushindi angalau katika mechi nne tu ili tuwe mabingwa na katika Kombe la FA tumeingia nusu fainali.

“Ingawa tukishinda mechi hizo tunaweza kutwaa ubingwa, nahitaji kuona tunapata ushindi katika michezo yote iliyobakia ya ligi na Kombe la Shirikisho. Hii itakuwa na maana kubwa kwa timu na naamini ni suala linalowezekana kwa sababu tuna timu nzuri na yenye ubora,” alisem.

Gomes alisema anafahamu kwamba wanakabiliwa na mechi ngumu na zenye ushindani katika ligi na mashindano ya Kombe la Shirikisho la Azam lakini wamejipanga kuhakikisha wanafanya vizuri katika harakati zao za kutetea makombe hayo mawili.

“Kila nyakati ninasema kuwa nina wachezaji wanaojitolea na wanajua wajibu wao na ninaona fahari namna wanavyojituma. Kile tunachoonyesha uwanjani hapana shaka ni cha kipekee, tumekuwa na muendelezo na kwa uhakika tunapaswa kuendelea hivyo.

“Kwa sasa Simba ni timu bora zaidi na naamini tuna nafasi ya kuchukua mataji yote mawili,” alisema Gomes.

Katika hatua nyingine Gomes alisema wanakwenda kwenye nusu fainali kucheza dhidi ya Azam Fc, ambayo ni moja ya timu ngumu yenye wachezaji bora na imara.

Alisema katika mechi ya kwanza ya ligi dhidi ya Azam Fc, uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2, ambao wachezaji wake walikosa nafasi nyingi za mabao pamoja na walitawala mpira.

“Mechi hiyo na Azam tulikuwa na kila sababu ya kushinda ila kuna makosa wachezaji wangu waliyafanya ambayo tukiyarekebisha nina imani kubwa tutashinda na kwenda kucheza fainali,” alisema.

“Azam ni moja ya timu ambayo msimu ujao itacheza mashindano ya kimataifa kwahiyo itakuja ikiwa imejipanga kutokana na ubora wetu ulivyo, tunawaheshimu lakini nina imani kubwa na wachezaji wangu, hawatafanya makosa kama mechi ya kwanza kwani tunataka ubingwa wa mashindana haya,” aliongeza kocha huyo kipenzi cha mashabiki wa Simba.

Katika Ligi Kuu, Simba imebakisha mechi tisa ambazo ni dhidi ya Namungo itakayocheza nayo mechi mbili, Ruvu Shooting, KMC, Polisi Tanzania, Yanga, Coastal Union, Azam FC na Mbeya City.