Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gamondi aibuka Kwa Mkapa kuisoma Simba

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi na  Meneja wa timu hiyo Walter Haryson wametinga katika Uwanja wa Mkapa kutazama mchezo wa Ligi kuu Bara kati ya Simba dhidi ya Ihefu.

Gamondi ameingia mapema kwenye uwanja nusu saa kabla ya mchezo huo kuanza na kushuhudia wachezaji wa timu hizo wakipasha misuli joto.

Gamondi amefika uwanjani kwa ajili ya kuwatazama wapinzani wao Simba ambao watakutana mchezo unaofuata Novemba 5 mwaka huu katika uwanja huo huo.

Kocha huyo amekuwa na utaratibu wa kwenda kutazama mechi wapinzani wao Simba kwani hata kwenye mchezo wa African Football League dhidi ya Al Ahly  alikuwepo uwanjani.