Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gadiel huyoo, atimkia Sauzi

ALIYEKUWA nahodha wa Singida Fountain Gate, Gadiel Michael anajiandaa kwenda Afrika Kusini kujiunga na kikosi cha Cape Town Spurs (Ajax Cape Town) iliyomnunua kupitia dirisha dogo, dili zima likiwekwa wazi na Rais wa timu hiyo, Japhet Makau alipozungumza mapema leo Jumanne.

Gadiel aliyewahi kuchezea Azam, Simba na Yanga anakwenda kuicheza Cape Town inayoshika nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu ya Sauzi, ni miongoni mwa wachezaji waliouzwa nje ya nchi huku ikiwa bado majina ya wengine hayawekwa wazi.

Makau amesema watu wasiwe na mshangao kwanini wanauza wachezaji wengi ila ni jambo la kawaida na mpira ni biashara kama zingine hivyo zikija ofa za kuhitaji wachezaji hawana budi kuwauza ili kujipatia pesa za kuleta wengine.

Rais huyo wa Singida, amesema miongoni mwa wachezaji waliouzwa nje ya nchi ni pamoja na Gadiel huku sita wengine wakienda Ihefu ambapo timu hizo ndizo zilizofikia makubaliano mazuri na uongozi wa timu hiyo unaomiliki wachezaji hao.

"Timu sasa imewatoa wachezaji wengi kwani tulitoa pesa nyingi sana ili kumalizana na kesi ya FIFA iliyokuwa inatukabili na ni vizuri kuwauza wachezaji ambao bado wako kwenye kiwango kizuri kwani ni faida kwa timu na hata kwa mchezaji," amesema Makau na kuongeza;

"Hakuna mgawanyiko wowote kama inavyosemekana, kwani kila kitu kuhusu Singida kiko vile vile na kikosi kilichobaki kina uwezo mkubwa wa kuzidi kushindana na ni uhakika kuwa tutasalia katika nafasi nzuri ndani ya ligi."

Singida iliyopanda Ligi Kuu Bara msimu uliopita ikiwa na jina la DTB kabla ya kubadilishwa kuwa Singida Big Stars kisha kuungana na Fountain Gate na kuwa Singida Fountain Gate, kwa sasa inashika nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu Bara nyuma ya KMC, Simba, Yanga na Azam inayoongoza kwa sasa.

Wachezaji iliyowaachia kwenda Ihefu ni Joash Onyango, Elvis Rupia, Marouf Tchakei, Kelvin Nashon, Bruno Gomes na kipa Abubakar Khomeny, japo kanuni inazuia wachezaji zaidi ya watano kutolewa kwa mkopo kutoka timu moja katika dirisha la usajili kwenda nyingine, labda kama walisajiliwa pia kwa mkopo.