Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fifa yamuongezea kibano Kwesi Nyantakyi

Zurich, Uswisi. Bosi wa zamani wa Chama cha Soka cha Ghana, Kwesi Nyantakyi, amezidi kuminywa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

Nyantakyi alilazimika kujiuzulu wadhifa wote wa kisoka kuanzia uongozi wa GFA pamoja na ule wa CAF  na Fifa, kutokana na kuibuliwa kwa madai ya kashfa ya rushwa na ufisadi dhidi yake.

Kiongozi huyo alihukumiwa kujiweka kando na masuala ya soka kwa siku 90 Juni 8 mwaka huu, ameongezewa siku nyingine 45 zaidi za adhabu.

Kamati ya maadili ya Fifa ilimkuta Nyantakyi na kosa la kupokea fedha zinazoaminika kuwa za rushwa ingawa yeye alijitetea kuwa hiyo ilikuwa zawadi kutoka kwa jamaa yake.

Alidaiwa kujichanganya kuhusu kiasi cha Dola 65,000 za Marekani alizobambwa nazo mwandishi wa habari, Anas Aremeyaw Anas, fedha ambazo alishindwa kuzitolea maelezo ya kina.