Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dodoma Jiji kung'oa kiungo Simba

UONGOZI wa Dodoma Jiji upo kwenye hatua za mwisho kutuma maombi kwa uongozi wa Simba kuona kama kuna uwezekano wa kumpata kiungo wa ukabaji, Victor Akpan aliyeshindwa kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza.

Akpan alisajiliwa na Simba kwenye dirisha kubwa la usajili msimu huu kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Coastal Union baada ya kuonyesha kiwango bora huko haswa msimu uliopita.

Taarifa zinaeleza benchi la ufundi la Dodoma Jiji chini ya kocha, Mellis Medo limeonyesha nia ya kuhitaji saini ya kiungo huyo hata kwa mkopo kwenye dirisha hili dogo la usajili.

Medo amewaeleza mabosi zake anahitaji wachezaji wachache wenye uzoefu ili kuongeza nguvu kikosini ili kuongeza makali ya timu hiyo haswa mzunguko wa pili ili kumaliza msimu vizuri tofauti na ilivyoanza.