Diarra kumfuata El Shanawy?

Muktasari:
- Swali kubwa ni ikiwa Diarra atafuata nyayo za golikipa wa Al Ahly Mohammed El Shenawy ambaye ndio alishinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mwaka 2022.
Golikipa wa Yanga amezua maswali kwa wadau mbali mbali baada ya kuchaguliwa kuwa mmoja ya mastaa wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wanaocheza ndani.
Swali kubwa ni ikiwa Diarra atafuata nyayo za golikipa wa Al Ahly Mohammed El Shenawy ambaye ndio alishinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mwaka 2022.
Ikiwa Diarra atashinda tuzo hii atakuwa amefuta nyayo za El Shanawy ambaye mwaka huu pia yupo kwenye orodha ya wachezaji wanaowania tuzo hii.
Mbali ya Diarra na El Shanawy, katika orodha hii pia kuna kipa wa Mamelod Sundown Ronwen Williams na kipa wa Wydad Casablanca Youssef El Motie.
Diarra ameingia kwenye orodha hii baada ya kuonyesha kiwango bora kwa msimu uliopita ambapo aliisaidia Yanga kufika fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika licha ya kupoteza mbele ya USM Alger.
Kwa upande wa makipa wenzake kuanzia kwa El Shanawy huyu ameingia hapa baada ya kufanya vizuri na Al Ahly na akaidaia kuchukua ubingwa wa Ligi ya Mabingwa kwa msimu uliopita na Williams wa Mamelod yeye aliifikisha timu yake robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.