Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diarra, Camara wavuta mamilioni FIFA


VIGOGO vya soka nchini Yanga na Simba kila moja inajiandaa kupiga noti kupitia kwa makipa Djigui Diarra na Moussa Camara huku Feisal Salum ‘Fei Toto’ akiendelea kuibeba Azam FC.


Fifa imetenga Dola 100 milioni za ziada kwa ajili ya kuzizawadia klabu zilizowaruhusu wachezaji kushiriki mechi za kufuzu Kombe la Dunia 2026.

Kutokana na jumla ya mechi 905 za kufuzu zilizochezwa duniani kote kabla ya mashindano hayo, klabu zinatarajiwa kupata wastani wa Dola 2,360 (Sh6.2 milioni) kwa kila mchezaji kwa kila mechi ya kufuzu aliyoshiriki.

Upanuzi wa mpango huo unamaanisha kuwa hata klabu za madaraja ya chini na ligi za ndani zitapata faida kubwa kifedha, hata kama wachezaji wao hawakufanikiwa kufika kwenye fainali za Kombe la Dunia.

Hapo ndipo Simba, Yanga na Azam zitavuna kutoka Fifa ni kutokana na kutumika zaidi makipa wao Diarra, Camara na kiungo Fei Toto kwa timu zao za taifa katika mechi za kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2026 ambalo linaanza rasmi Alhamisi, wiki ijayo katika nchi za Mexico, Canada na Marekani.

Malipo hayo yatahusu mchezaji aliyetumika kwa kucheza mchezo husika au kuwemo katika orodha ya wachezaji wa akiba.

Diarra amecheza mechi tano za kufuzu Kombe la Dunia za Mali ambazo zitaifanya Yanga ivune kiasi cha Dola 11,800 (Sh31 milioni) huku Camara akiwa Simba aliitumikia Guinea katika mechi sita hivyo ataiingizia Dola 14,160 (Sh37 milioni) kiasi ambacho pia Fei Toto ataiingizia Azam FC.

Katika orodha ya wachezaji watakaoingiza kiasi kikubwa cha fedha kwa klabu hizo, kinara ni Ibrahim Hamad ‘Bacca’ wa Yanga ambaye ataifanya timu yake kuvuna Dola 16,520 (Sh43 milioni).

Kwa ujumla, Yanga inaonekana itavuna kiasi kikubwa cha fedha kutoka Fifa kwani idadi kubwa ya wachezaji walishiriki mechi nyingi za kuwania kufuzu Kombe la Dunia wakiwa na timu tofauti za taifa.

Timu hiyo itavuna zaidi ya Dola 141,600 (Sh372 milioni), Simba itapata zaidi ya Dola 129,800 (Sh341 milioni) na Azam itapata zaidi ya Dola 118,000 (Sh310 milioni) kutoka gawio.

Klabu nyingine za Tanzania ambazo zitanufaika na mgawo huo wa Fifa kwa kutoa wachezaji ambao wamezitumikia timu za taifa katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia 2026 ni Singida Black Stars, Dodoma Jiji, Coastal Union, TRA United pamoja na JKT Tanzania.

Kwa ujumla Dola 250 milioni zitatolewa na Fifa kwa klabu mbalimbali duniani ambazo  wachezaji wanashiriki katika fainali za Kombe la Dunia zijazo.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Fifa, kiwango cha chini kinachotarajiwa kulipwa kwa klabu ni takribani Dola 5,000 kwa kila mchezaji kwa siku.

Malipo ya mwisho yatazingatia kwa umakini muda halisi ambao kila mchezaji atashiriki kwenye mashindano hayo, kuanzia hatua ya makundi hadi raundi za mtoano.

Hata hivyo, klabu duniani zinatarajiwa kupata sehemu kubwa zaidi ya fedha hizo kutokana na kuwa na idadi kubwa ya wachezaji wa kimataifa wanaoshiriki mashindano hayo.