Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

De Ligt anakaribia kutua Juventus

Muktasari:

Manchester United na Paris Saint-Germain nazo zilikuwa zikimfukuzia De Ligt, lakini beki huyo kinda mwenye umri wa miaka 19 ameamua kwenda kujiunga na Juventus.

TURIN, ITALIA.BEKI, Matthijs de Ligt amedaiwa kuwa kwenye hatua za mwisho kabisa za kukamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Juventus baada ya kugomea kujiunga na kambi ya mazoezi ya timu ya Ajax.
Mwandishi wa habari wa huko Uholanzi, Mike Verweij alisema beki huyo wa kati anayesakwa kila kona huko Ulaya, ameachwa kando kwenye kikosi cha Ajax kilichokwenda Austria kwa ajili ya kuweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya na jambo hilo linadaiwa kwamba amefanya hivyo kwa sababu anakamilisha mambo yake ya kuhamia Juventus.
Manchester United na Paris Saint-Germain nazo zilikuwa zikimfukuzia De Ligt, lakini beki huyo kinda mwenye umri wa miaka 19 ameamua kwenda kujiunga na Juventus.
Juzi Ijumaa, Verweij alituma ujumbe kwenye Twitter uliosomeka: "Matthijs De Ligt hayupo kwenye kambi ya Ajax huko Austria kwa sababu anataka kukamilisha uhamisho wake."
Kisha akatuma ujumbe mwingine: "Ajax na Juventus zimekubaliana ada ya uhamisho wa Matthijs De Ligt. Kila kitu sasa kimekaa kwenye mstari. Uhamisho unakamilika."
Juventus wanadaiwa kupeleka ofa ya Pauni 58.3 milioni kunasa huduma ya Mdachi huyo, huku Pauni 49.3 milioni ikitangulizwa na nyingine zitakuwa nyongeza za baadaye.
Supastaa, Cristiano Ronaldo amedaiwa kuhusika kwenye usajili huo wa De Ligt baada ya kumshawishi akajiunge Turin baada ya kukutana kwenye fainali ya Uefa Nations League iliyozikutanisha Ureno na Uholanzi.
Mapema wiki iliyopita, wakala wa beki De Ligt, Mino Raiola, alithibitisha kukamilika kwa makubaliano na Juventus.