Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

De Gea katika kashfa ya picha za ngono

Kipa wa Manchester United, David de Gea.

Muktasari:

Ripoti ya polisi ilidai kwamba shahidi mmoja wa siri katika kesi inayomkabili mtayarishaji picha za ngono, Ignacio Allende au Torbe, alidai kwamba mwaka 2012, De Gea alipanga naye ahadi pamoja na

MADRID, HISPANIA
KIPA wa Manchester United, David de Gea anachunguzwa na polisi baada ya kuhusishwa katika kashfa ya kusimamia mtandao wa ukahaba uliohusisha watoto wa wadogo.
Ripoti ya polisi ilidai kwamba shahidi mmoja wa siri katika kesi inayomkabili mtayarishaji picha za ngono, Ignacio Allende au Torbe, alidai kwamba mwaka 2012, De Gea alipanga naye ahadi pamoja na msichana mwingine na wachezaji wawili wa timu ya vijana chini ya miaka 21 ya Hispania.
Hata hivyo habari kutoka kwa mtu aliye karibu na kipa huyo zilidai kwamba hajashitushwa na habari hizo, amezipinga vikali na ameendelea na mambo yake kama kawaida akiamini ataendelea kuwa na timu ya Hispania nchini Ufaransa kwenye fainali za Euro 2016.
Torbe alikamatwa na kutiwa ndani Aprili mwaka huu baada ya kudaiwa kuendesha mtandao wa makahaba akitumia zaidi wasichana wa umri mdogo kwa ajili ya kuwapiga picha.
Shahidi huyo wa siri alisema kwamba alifanyiwa udhalilishaji wa kijinsia na wanasoka wawili katika hoteli moja ya nyota nne ya mjini Madrid.
Alifafanua kwamba wachezaji hao wawili waliokuwa na timu ya vijana chini ya miaka 21 wakati huo, De Gea hakuwamo.
Taarifa zaidi nchini Hispania zilidai kwamba mmoja wa wachezaji hao ni mshambuliaji wa Athletic Bilbao, Iker Muniain lakini msichana huyo hakuweza kumtambua mchezaji wa pili zaidi ya kusisitiza kwamba mpango huo wa kukutana ulipangwa na De Gea na Torbe.
Shahidi huyo alifafanua kwamba, Torbe alimpakiza kwenye gari lake na kumpeleka katika hoteli ambayo alikutana na wachezaji hao na mwanamke mwingine na akatakiwa kufanya nao chochote walichotaka na kuonywa asitoe siri ingawa fedha alizoahidiwa hakupewa.
Klabu ya Manchester United imekata kulizungumzia suala hilo. De Gea anayetajwa kuwa mmoja wa makipa bora duniani anajulikana akiwa na uhusiano wa kimapenzi na mrembo mwanamuziki, Edurne Garcia ambaye wamekuwa pamoja kwa takriban miaka sita sasa.

Kwa taarifa zaidi nunua gazeti lako la Mwanaspoti au soma mtandaoni kupitia www.epaper.mcl.co.tz