Coastal yaitangulia Yanga mapemaa
Timu ya Coastal Union imetangulia mapema uwanjani, kujiandaa na mchezo wao wa Ligi Kuu NBC dhidi ya Yanga katika uwanja wa sheikh Amri abeid Arusha.
Coastal union imeingia saa 7:50 uwanjani tofauti na ilivyozoeleka kuingia saa nane kujiandaa na mchezo wa saa kumi dhidi ya Yanga.
Yanga nao wameingia uwanjani hapo saa 8:40 nyuma ya wenyeji wao huku wakipokelewa na shagwe na nderemo kutoka kwa mashabiki wao.
Yanga na Coastal zinatarajia kucheza mchezo huo wa pili wa ligi, wote wakiwa na kiu kubwa ya kuhakikisha wanaendeleza ushindi walioupata katika mchezo wa awali.
Awali Yanga iliibuka na Ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania huku Coastal wakiondoka na alama tatu dhidi ya MKC kwa bao 1-0 katika uwanja wa Sheikh Amri abeid.
Kiingilio katika mchezo huo mzunguko ni shilingi 7000 na VIP A na B ni 10,000 huku VVIP ni shilingi 30,000.