Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Coastal hawana chao Sheikh Amri Abeid

Coastal hawana chao Sheikh Amri Abeid

Muktasari:

  • Coastal Union inatarajia kushuka dimbani leo saa kumi katika mchezo wa pili wa Ligi Kuu NBC dhidi ya Yanga wote wakiwa wamevuna alama tatu katika michezo ya awali.

Arusha. KLABU ya Coastal Union ya Tanga, inatarajia kushuka dimbani leo saa kumi dhidi ya mabingwa watetezi Yanga huku wakikosa mkwanja wa kuuza jezi zao.

Mchezo huo unaotarajia kupigwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, wafanyabiashara wamechangamkia fursa kwa kuupamba uwanja huo kuuza jezi za timu mbali mbali ikiwemo za Yanga, Simba na Azam FC.

Mmoja wawafanya biashara wa jezi nje ya uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Athumani Ally amesema kuwa ingawa coastal wanacheza leo lakini wamekosa jezi zao kwa ajili ya kuziuza.

"Mimi sijawahi kuuza jezi za Coastal Union lakini kuna baadhi ya wenzangu juzi kwenye mechi ya awali dhidi ya KMC walikuwa nazo naona leo hawapo." alisema Ally.

Alisema kuwa jezi zinazoongoza kwa mauzo ni za Yanga na Simba pekee huku jezi mpya zikifanya vizuri zaidi.

"Jezi mpya za Yanga zinachangamkiwa haswa ambayo tunauza 35,000 na hizi za zamani pia zinatoka kwa bei ya 20,000 lakini kwa uchache." aliongeza Ally.