Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CAF yaibeba Yanga, yatoa angalizo kwa Twite na Oscar

Pichani ni beki wa Yanga, Mbuyu Twite

Muktasari:

Miongoni mwa wachezaji hao imeonya kwamba wakitumia wanaweza kupata nuksi na wasicheze mechi ijayo mjini Harare.

KOCHA wa Yanga, Hans Pluijm amewataka wachezaji wake kusahau yaliyowatokea katika mchezo wao uliopita dhidi ya Simba na kuelekeza nguvu zao dhidi ya Platinum ya Zimbabwe, lakini CAF imeionyesha nia nzuri ya kutaka Yanga isiingie mkenge baada ya kutuma taarifa fupi ikiionya timu hiyo juu ya wachezaji wake watatu.

Miongoni mwa wachezaji hao imeonya kwamba wakitumia wanaweza kupata nuksi na wasicheze mechi ijayo mjini Harare.

Yanga ambayo itashuka katika Uwanja wa Taifa Jumapili kucheza na Platinum, katika mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho, imetumiwa taarifa hiyo ikionywa juu ya matumizi ya wachezaji hao ambao wawili ni mabeki wa pembeni na mmoja akiwa mshambuliaji.

Katibu Mkuu wa Yanga, Dk. Jonas Tiboroha ameliambia Mwanaspoti kuwa CAF (Shirikisho la Soka la Afrika) limewapa tahadhari kwa Oscar Joshua anayecheza beki wa kushoto na Mbuyu Twite anayecheza kulia kuwa tayari wana kadi ambazo walizipata katika mchezo uliopita dhidi ya BDF ya Botswana.

Tiboroha alisema CAF imewaambia kuwa Oscar alifanya makosa ya kuchelewesha mchezo kwa kuzembea kurusha mpira kwa wakati na Twite alipewa kadi hiyo kwa kumchezea rafu kiungo wa BDF na endapo watafanya makosa kwa kupewa kadi za njano dhidi ya Platinum wanaweza kukaa jukwaani katika mchezo wa marudiano. Danny Mrwanda alipata kadi nyekundu.

“Tunajua kwamba mchezo dhidi ya Platinum utakuwa mgumu lakini tunataka kuwaelekeza wachezaji wetu jinsi ya kuwa makini katika kutoruhusu makosa kama hayo ambayo yanaweza kuwakosesha mchezo ujao.”

MHOLANZI

ANAJUA KIKOSI

Mashabiki wa Platinum wanaanza safari leo Alhamisi kwa basi kuja Dar es Salaam kuishangilia timu yao na watarejea Zimbabwe Jumatatu.

Timu huenda ikawasili leo mchana kwa ndege ya Shirika la ndege la Kenya ambalo nauli yao ni Sh1.3 milioni kwenda na kurudi kwa mtu mmoja.

Kocha wa Yanga, Hans Pluijm amewakomalia mabeki wake akiwataka kuongeza umakini vinginevyo safari yao inaweza kuishia Zimbabwe.

Alisema: “Tunatakiwa kuwa makini wakati wote, tunatakiwa akili zetu tuzitulize uwanjani hasa kwa watu wa ulinzi hatutakiwi kufanya makosa ya kuwapa nafasi hawa wageni kupata goli lolote hapa nyumbani.”

“Najua soka ni mchezo ambao huwezi kucheza kwa uwezo wako bora kila siku lakini tumefanya makosa katika mchezo uliopita sasa tusahau, tunatakiwa kushinda mechi yetu ijayo nafasi hiyo tunayo.”

Yanga itaingia kwenye mchezo huo ikijaribu kusahau kipigo cha bao 1-0 ilichokipata mbele ya Simba katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa Uwanja wa Taifa Jumapili iliyopita.