Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bruno bado hajajipata Singida

Muktasari:

  • Bruno aliyekuwa kinara wa mabao wa Singida msimu uliopita akifunga mabao 10, alienda kuoa kwao Brazili na alichelewa kujiunga na kambi ya maandalizi ya msimu mpya na kujikuta akishindwa kutumika kwenye mechi zote ilizocheza timu hiyo kuanzia zile za kirafiki za kimataifa hadi mechi ya CAF.

KIUNGO fundi wa Singida Fountain Gate kutoka Brazili, Bruno Gomes amesema ana kazi kubwa ya kufanya kurudisha ubora wake wa msimu uliopita baada ya kukiri kuchelewa kujiunga na timu kumemrudisha nyuma kiasi kwamba hadi sasa bado anajitafuta.

Bruno aliyekuwa kinara wa mabao wa Singida msimu uliopita akifunga mabao 10, alienda kuoa kwao Brazili na alichelewa kujiunga na kambi ya maandalizi ya msimu mpya na kujikuta akishindwa kutumika kwenye mechi zote ilizocheza timu hiyo kuanzia zile za kirafiki za kimataifa hadi mechi ya CAF.

Akizungumza na Mwanaspoti, Bruno alikiri ana kazi kubwa ya kujitafuta hadi ajipate kurejea kwenye makali aliyokuwa nayo katika msimu wa kwanza na kikosi hicho cha Big Stars.

“Nimejiunga na timu kwa kuchelewa bado sipo imara zaidi, lakini naamini hilo haliwezi kuniondoa mchezoni naamini nina muda na nafasi ya kuonyesha kile nilichonacho. Usajili uliofanyika unaniongeza changamoto ya kupambana zaidi na utanipa nguvu ya kuniongezea ubora kutokana na kuhitaji nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza,” alisema Bruno.


MSIKIE PLUIJM
Kocha Mkuu wa Singida, Hans Pluijm amesema upana wa kikosi alichonacho unamfanya apate ugumu kupata kikosi cha kwanza hadi sasa kutokana na ubora na viwango unaofanana kwa wengi wao.
Pluijm alisema uongozi kwa kushirikiana naye wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupata timu nzuri na ya ushindani kazi iliyobaki sasa ni namna atakavyopata kikosi cha kumpa matokeo.

“Nina kikosi kipana chenye wachezaji 31 ubora wa wachezaji kwa asilimia kubwa unalingana hadi muda huu sina kikosi cha kwanza kwasababu nafanya kujaribu nani ataweza kuwa bora zaidi ya mwingine. Sio rahisi lakini napambana ninachofurahia zaidi ni kwamba kila mchezaji ninayempa nafasi anapambana tupate matokeo hilo ndio la muhimu zaidi,” alisema kocha huyo wa zamani wa Yanga na Azam.