Bosi Yanga apiga mkwara, hakuna wa kuwashusha

Muktasari:
- Hersi Said, rais wa Yanga ameyasema hayo makao makuu ya klabu alipokuwa akizungumza na nyomi ya mashabiki waliojitokeza kufurahia ubingwa ilioupata timu yao.
Uongozi wa klabu ya Yanga umeahidi usajili bora zaidi msimu ujao na kuweka wazi kuwa hakuna timu ya kuwashusha kwa mafanikio waliyoyapata misimu minne mfululizo.
Hersi Said, rais wa Yanga ameyasema hayo makao makuu ya klabu alipokuwa akizungumza na nyomi ya mashabiki waliojitokeza kufurahia ubingwa ilioupata timu yao.
Hersi amesema wachezaji walioondoka na watakaondoka wao kama viongozi watafanya usajili mwingine bora zaidi ili kuendeleza mafanikio waliyoyapata.
“Hakuna timu ya kutushusha tumefika kwenye kilele cha mafaniko, tutaendelea kuwa bora msimu ujao. Tulipofika misimu minne iliyopita msimu ujao tutaendelea hapo,” amesema na kuongeza:
“Hatuwezi tukawa bora kwa misimu minne tukarudi kwenye shida msimu ujao. Tutarudi tukiwa imara na kuendeleza ubora ili kuendeleza ushindani.”