Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bosi Mtibwa Sugar aweka mikakati mipya

MTIBWA Pict

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwanaspoti, Swabri alisema haamini kitendo cha yeye kurudi katika timu hiyo ndio sababu ya kurejea tena Ligi Kuu Bara, isipokuwa utulivu na mikakati ya viongozi kwa ujumla ilifanikisha kutimiza malengo waliyojiwekea mwanzo.

KITENDO cha Mtibwa Sugar kurejea Ligi Kuu Bara baada ya kushuka msimu uliopita, kimemfanya ofisa mtendaji mkuu wa kikosi hicho, Swabri Aboubakar kueleza sababu iliyochangia mafanikio hayo ni ushirikiano wa viongozi na wala sio vinginevyo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Swabri alisema haamini kitendo cha yeye kurudi katika timu hiyo ndio sababu ya kurejea tena Ligi Kuu Bara, isipokuwa utulivu na mikakati ya viongozi kwa ujumla ilifanikisha kutimiza malengo waliyojiwekea mwanzo.

“Sitaki kusema mimi ndio sababu ya timu kupanda kwa sababu tumeshirikiana kama klabu, kazi ilikuwa ni ngumu kutokana na ugumu na ushindani uliopo, hivyo tunajipanga kuhakikisha msimu ujao tunaleta ushindani zaidi ya huu,” alisema Swabri.

Swabri anayeiongoza Mtibwa ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara mwaka 1999 na 2000, alisema ni mapema kuzungumzia mikakati watakayokuja nayo, ingawa mashabiki wa timu hiyo watarajie mambo mazuri, kuanzia usajili mzuri wa kurejesha heshima yao.

Mtibwa imerejea Ligi Kuu Bara ikiungana na Mbeya City iliyoshuka msimu wa 2022-2023, baada ya timu hizo kujihakikishia kumaliza nafasi ya kwanza na ya pili katika msimamo wa Ligi ya Championship, kutokana na mwenendo mzuri tangu mwanzoni.

Swabri aliondolewa kikosini humo Desemba 29, 2023 na nafasi yake ikachukuliwa na Abdulrahman Joshi, ingawa baada ya timu hiyo kushuka daraja kutokana na mwenendo mbaya katika Ligi Kuu Bara msimu uliopita, viongozi wakamrejesha tena kundini.