Bondia Joshua aingizwa mtegoni
Muktasari:
- Golovkin mwenye miaka 36 ametawala ngumi za uzani wa Middle tangu mwaka 2010 – 2018 akishikilia mataji ya WBA (Super Middle), WBC, IBF, na IBO (Middle) na anadhani kwa sasa hana mpinzani katika uzani huo.
Los Angeles, Marekani. Bondia Gennady Golovkin raia wa Kazakhstani amesema baada ya kumshinda Canelo Alvarez raia wa Mexico sasa atapanda uzito ili acheze na Anthony Joshua katika uzani wa juu.
Baada ya wikiendi iliyopita kumshinda Alvarez na kutetea mataji yake yote Golovkin ambaye hajapoteza pambano tangu mwaka 2010 alisema kuwa atazungumza na kocha wake ili aongeze uzito.
“Sidhani kama ninapaswa kuendelea kucheza katika uzani huu ambao sina mpinzani, uamuzi mzuri wa kufanya ni kubadili uzani ninadhani katika hilo rahisi ni kuongeze uzito ili nicheze uzani wa juu,” alisema.
Baada ya kutangaza hilo mwandishi wa ngumi Vasyl Lomachanko alisema iwapo Golovkin ataamua kupandisha uzito atakuwa na nafasi kubwa ya kutawala kwani kwa sasa mabondia wa uzani wa juu hakuna mtaalamu wa masumbwi.
Amemshauri kutofikiria kucheza na Anthony Joshua, ambaye hayupo katika kumi bora ya mabondia bora wa uzani wa juu, badala yake aombe kucheza na Vasyl Lomachenko wa Ukraine aliyependekezwa kuwania ubingwa wa Dunia.