Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bodi ya Filamu yaandaa rasimu kuwabana wanyonyaji

Muktasari:

  • Akiwa mkoani hapa katika warsha ya kuwajengea wadau wa tasnia hiyo kuwa na uwezo wa kutoa filamu ambayo itakuwa inauzika sio Tanzania pekee kutokana na maudhui yatakayopatikana kwenye filamu husika.

Arusha: Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fissoo ameeleza kuwa wapo katika mchakato wa kupokea maoni ya kuwabana watu wanaokula jasho la waigizaji kwa njia zisizo halali.
Akiwa mkoani hapa katika warsha ya kuwajengea wadau wa tasnia hiyo kuwa na uwezo wa kutoa filamu ambayo itakuwa inauzika sio Tanzania pekee kutokana na maudhui yatakayopatikana kwenye filamu husika.
“Kanuni ya mwaka 1976 ambayo ilirekebishwa mwaka 2011 zinatambua miundombinu na maeneo ya kuoneshea filamu kama moja ya fulsa ya kutanua tasnia.”
“Serikali kupitiua wizara husika imetuagiza bodi ya filamu kutengeneza kanuni mahsusi kwaaaji ya kudhibiti vibanda vya kuoneshea filamu ikiwa ni moja ya fulasa kwa wadau kuanza kunufaika na kazi zao,” alisema Fisso.
Aliongeza kuwa tayari wamepita mikoa kadhaa katika ukusanyaji wa maoni ikiwemo Morogoro, Mwanza, Mara, Shinyanga, Arusha na Mtwara na kabla ya mwezi wa tano watakuwa wameshafika Mikoa ya Kigoma Geita, Songwe na Manyara.
 
Alisema hadi Mei Mosi wanatarajia kukamilisha rasimu ya kwanza kabla ya kwenda kujadiliwa kwenye wizara na hatimaye kupelekwa kwa wadau ili kuichambua tena na kufanya zoezi hilo kuwa endelevu.
Aliongeza kuwa katika kuhakikisha wanaweka usawa wamekutana na kujadili pamoja na wamiliki wa vibanda vya kuoneshea filamu ili waweze kuonesha angalau filamu mbili kwa siku za Tanzania na kusajiliwa rasmi.
“Mtayarishaji, muongozaji na mwandishi wote lazima awe na taaluma (maarifa na stadi) ya uwezo kuanziasha wazo, kuratibu, kusimamia, kudhibiti mambo ya kama ya upatikanaji wa fedha/ mtaji, kuajiri watendaji wakuu kwenye utengenezaji wa filamu, kuingia mikataba na wasambazaji.”
Pia alisema kuwa tasnia hiyo imefanikiwa kwa kuongezeka kwa wasambazaji wa filamu kutoka mmoja mwaka 2004/2005 hadi kufikia 139 mwaka 2016.