Bodaboda zapiga dili Wananchi wakifuata tiketi

Saturday August 06 2022
boda pic
By Thomas Ng'itu

BAADA ya kitendo cha tiketi kuuzwa katika eneo la Gwambina Lounge, Temeke imewapa fursa madereva wa bodaboda kufanya biashara ya kuwabeba mashabiki wa Yanga kufuata tiketi hizo.

Awali tiketi huwa zinauzwa katika uwanja wa Uhuru lakini leo eneo hilo haziuzwi badala yake zinapatikana Gwambina Lounge.

Mashabiki walionekana kupata tabu ya upatikanaji wa tiketi na walipouliza, bodaboda waliwaambia ; ”Panda nikupeleke utanipa buku”

Mashabiki walikuwa na ulazima wa kufanya hivyo kutokana na uhitaji wa kuingia uwanjani mapema ili kushuhudia kilele cha Siku ya Mwananchi.

Mwanaspoti lilifika hadi Gwambina Lounge na kushuhudia bodaboda nyingi zikiwa zimepaki nje ya geti zikisubiri wateja waliowaleta.

Upande wa tiketi  ndani  foleni ilikuwa sio kubwa sana hali iliyowafanya mashabiki waingie ndani na kutoka nje baada ya kufanikiwa mahitaji yao.

Advertisement
Advertisement