Bodaboda asepa na Sh51 milioni
Mkazi wa Kimara Peter Patric ameibuka kidedea akijishindia kiasi cha sh 51.1 milioni kupitia michezo ya kubashiri.
Patric ambaye ni dereva wa pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda amejishindia fedha hizo Jana kufuatia kupatia matokeo ya mechi 50 kupitia kampuni ya Premier Bet.
Akizungumza wakati wa makabidhiano wa fedha hizo Patric amesema ameshinda fedha hizo akitumia dau la Sh2,150 tu.
Hata hivyo mara baada ya ushindi huo Patric aliwavunja mbavu waandishi wa habari akidai kama Kuna mechi iliyokuwa inampa presha katika mechi alizochagua basi ni Ile ya Bayern Munich ya Ujerumani.
"Nimekuwa nikishinda lakini kiasi cha fedha cha kawaida sana ila huu ndio ushindi wangu wa kihistoria mpaka Sasa,"alisema Patric.
"Fedha hizi najipanga kwenda kujiendeleza zaidi kibiashara mimi ni dereva wa boda boda lakini Sasa nataka kwenda kufungua biashara ya vipodozi."