Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bingwa AFL kupatikana leo, Mamelodi vs Wydad

PRETORIA, AFRIKA KUSINI. MASHABIKI wa soka barani Afrika kuanzia saa 10:00 jioni watakuwa bize kufuatilia pambano la pili la fainali ya African Football League wakati Mamelodi Sundowns itakapokuwa nyumbani kurekebisha makosa ya mechi ya mkondo wa kwanza mbele ya Wydad Casablanca ya Morocco.

Katika mechi ya kwanza wikiendi iliyopita, Wydad ikiwa nyumbani, ilishinda 2-1 na kujiweka nafasi nzuri ya kuandika historia ya kuwa bingwa wa kwanza wa michuano hiyo, iwapo itashikilia bomba kwenye Uwanja wa Loftus Verfeld, mjini Pretoria.

Ushindi hata wa bao 1-0 unaweza kuwabeba wenyeji, lakini kwa jinsi Wydad ilivyoupiga mwingi kwenye michuano hiyo hadi sasa ni wazi, Mamelodi wana kazi ya ziada kama inataka kulibeba taji hilo ambalo Wekundu wa Msimbazi, Simba walishiriki na kung’olewa na Al Ahly.

Huo ni mchezo wa 14 kwa timu hizo kukutana kwenye michuano ya CAF, huku Wydad ikiwa na rekodi nzuri.