Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baraza atoa neno Lwasa akitimkia Angola

Muktasari:

  • Lwasa aliyezaliwa Novemba 5,1998, nchini Uganda alichambuliwa na kocha Baraza aliyemfundisha Pamba,kwamba kwa nidhamu na bidii yake anaamini atakwenda kufanya makubwa Angola.

BAADA ya kiungo mshambuliaji aliyemaliza mkataba wake na  Pamba Jiji, Peter Lwasa kujiunga na klabu ya G.D Interclube  ya Angola, kocha Francis Baraza anaamini atakwenda kufanya makubwa nchini humo.

Lwasa aliyezaliwa Novemba 5,1998, nchini Uganda alichambuliwa na kocha Baraza aliyemfundisha Pamba,kwamba kwa nidhamu na bidii yake anaamini atakwenda kufanya makubwa Angola.

"Lwasa ni mchezaji anayekubali kufundishwa ni mwanafunzi mzuri,sina wasiwasi alikokwenda kucheza ataendeleza utulivu,nidhamu,kupenda kujifunza kwa makocha anaokwenda kukutana nao huko," alisema Baraza na kuongeza;

"Ni mchezaji anayependa chalenji ya ushindani, atafanya vizuri zaidi ya kile alichokionyesha Ligi Kuu Bara kwa misimu aliyocheza hapa."

Lwasa ambaye msimu wa 2024/25 akiwa na Kagera Sugar alimaliza na Mabao manane kabla ya kuja Tanzania baadhi ya timu alizozichezea ni KCCA FC,Gor Mahia ya Kenya, Kariobangi, Sofapaka na URA.

Jambo ambalo Baraza alisema:" Lwasa ni mchezaji mwenye njaa ya mafanikio, anapenda kujaribu kupambana bila kukata tamaa, kutokana atafika mbali na atakuja kuishi ndoto zake anazozitamani kwenye maisha yake ya mpira wa miguu."

Baraza alisema mbali na Lwasa, wachezaji wote wa Pamba wanafanya kazi nzuri na wengi wao anawaona watafika mbali endapo wakiendeleza nidhamu na kujituma kwa bidii.