Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bao la Yacouba lawajaza

Muktasari:

YANGA imerejea jijini Dar es Salaam wakitokea Tabora walipokata tiketi ya kutinga hatua ya Fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC), lakini nyuma yake wakachukua tena mamilioni ya kibabe kutoka kwa matajiri wao.

YANGA imerejea jijini Dar es Salaam wakitokea Tabora walipokata tiketi ya kutinga hatua ya Fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC), lakini nyuma yake wakachukua tena mamilioni ya kibabe kutoka kwa matajiri wao.

Yanga imetinga hatua ya fainali ya ASFC kwa mara ya pili wakirudia kama walivyofanya mara ya mwisho mwaka 2016 walipotwa taji hilo kwa mara ya kwanza na ya pekee kabla ya kurudia tena juzi na ushindi wao wa bao 1-0 dhidi ya Biashara United umewaneemesha wachezaji wa timu hiyo.

Iko hivi. Yanga baada ya kushinda kwa bao lililofungwa na mshambuliaji Yacouba Songne wachezaji wa timu hiyo wamejihakikishia kuvuna kiasi cha sh 40 milioni.

Fedha hizo zilikuwa ni ahadi kutoka kwa matajiri wao ambapo Mwanaspoti linafahamu tajiri wa GSM, Ghalib Mohamed aliwatamkia mkwanja huo na jamaa wakafanya kweli.

Tayari Mwanaspoti linafahamu kwamba mapema Ghalib aliwapa ahadi ya kuwapa sh 300 milioni wachezaji wa timu hiyo endapo watalichukua taji hilo linaloshikiliwa kwa sasa na Simba watakaokutana nao kwenye fainali itakayopigwa Julai 25, mjini Kigoma.

Ahadi hiyo pia inaweza kupanda wakati wowote kutokana na kukutana kwao na Simba, iliyoinyoa Azam FC kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa nusu fainali nyingine uliopigwa mjini Songea, Ruvuma katika kuwapa morali zaidi wachezaji wa timu hiyo katika mechi ya watani.

Yanga imerejea juzi ambapo wachezaji wa timu hiyo watapewa mapumziko ya siku chache kabla ya kuingia katika maandalizi ya kukutana na Simba katika mchezo wa ligi, utakaopigwa Julai 3.

Mechi hiyo inarudiwa baada ya Mei 8 kushindwa kufanyika kutokana na utata wa kuahirishwa kwake saa 2 kabla ya kvaana kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.