Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bandari, Congo aibu tupu!

Waziri Mkuu, Raila Odinga (aliyevaa kofia) akiwa na wawakilishi wa klabu za soka za Kilifi baada ya kuwapa mipira kwenye sherehe fupi iliyofanyika Uwanja wa Kilifi. PICHA NA GEORGE KIKAMI

MWANDISHI WETU BANDARI na Congo zimeumbuka kwenye Ligi Kuu ya Kenya wikiendi iliyopita na kila moja imetoa utetezi wake ambao mashabiki wameusikia wakatikisa vichwa. Bandari ilifungwa mabao 1-0 na Mathare huku Congo ikichapwa bao 2-1 na Karuturi. Kocha wa Bandari Rishadi Shedu licha ya kusema kwamba hakustahili kufungwa amedai pia kwamba wachezaji wake walipania mno wakashindwa dhidi ya Mathare United kwenye uwanja wa Mbaraki Sports Club, Jumamosi iliyopita. Shedu; "Nitawaambia wawe makini na wasipanie sana bali wacheze mpira wao na kutumia vizuri nafasi. Haikuwa haki kwetu kushindwa kwani wachezaji wangu walicheza vizuri sana lakini walitupa nafasi zote walizopata hali wapinzani wetu walipata nafasi moja na wakaitumia." Naye mshambuliaji wa Bandari, Abdulwahab Mussa amesema kwamba walistahili kushinda pambano hilo lakini bahati na kupoteza kwao nafasi karibu nne za kufunga ziliwapa wapinzani wao ushindi walipotumia nafasi yao moja. Mkurugenzi wa Ufundi wa Congo United, Aref Baghazally alisema anashangazwa na matokeo hayo kwani alitegemea ushindi mkubwa. ìMabao ya Karuturi waliyoyapata kibahati, yaliwavunja nguvu wanasoka wetu,î akasema Baghazally. Naye nahodha wa Congo, Ramadhan Athman Mbuggus ; "Hii ni kawaida kwa soka kwani tulijitahidi angalau kupata pointi moja lakini haikuwa siku yetu." Kocha wa Mathare United, Salim Ali alisema ushindi walioupata ugenini ulikuwa ni wa mafanikio makubwa. Congo ilicheza chini ya kiwango tofauti na ilivyokuwa dhidi ya Gor Mahia iliposhinda kwa penati 10-9 katika mashindano ya Kombe la FKL.