Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baleke, Mayele wabeba matumaini ya mashabiki

Muktasari:

  • Simba inakutana na Yanga leo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 11:00 jioni huku vijiwe mbalimbali vya mashabiki waliojitokeza wakiwa na imani kubwa kupitia mastaa hao.

MASHABIKI wa Simba na Yanga wamekuwa na matumaini makubwa ya kuibuka na ushindi katika mchezo wa 'Kariakoo Derby' huku nyota wanaotajwa zaidi ni Fiston Mayele na Jean Baleke.

Simba inakutana na Yanga leo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 11:00 jioni huku vijiwe mbalimbali vya mashabiki waliojitokeza wakiwa na imani kubwa kupitia mastaa hao.

Shabiki wa Simba, Simon Samwel amesema kiwango kizuri anachokionyesha Baleke kinawafanya kuamini watashinda.

"Michezo hii huwa siku zote haitabiriki lakini awamu hii naiona kabisa tukishinda kwa sababu wenzetu wanajiamini kupitiliza jambo ambalo naliona kwao litawagharimu.," amesema.

Kwa upande wa shabiki wa Yanga, Nurath Osman amesema wana kila sababu za kushinda kutokana na rekodi waliyonayo kwa wapinzani wao.

"Sisi tunataka kuchukua ubingwa na ili tufurahie zaidi ni lazima tumfunge mpinzani wetu baada ya kumkosa mzunguko wa kwanza."

Mayele ndiye kinara wa ufungaji bora katika Ligi Kuu Bara akiwa na mabao 16 huku Baleke akiwa na mabao saba.

Simba na Yanga zinakutana tena baada ya mchezo wa kwanza uliopigwa Oktoba 23, mwaka jana timu hizo kufungana bao 1-1.