Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baada ya kichapo, Reel Dream yarudisha mzuka

Muktasari:

  • Maria aliliambia Mwanaspoti, morali imerudi baada ya kupoteza mechi ya kwanza  dhidi ya Tausi Royals kwa pointi 58-55.

BAADA ya Reel Dream kuifunga Ukonga Queens kwa pointi 70-54, katika Ligi ya kikapu Dar es Salaam (WBDL), nyota wa timu hiyo Maria Boniventura  amesema ushindi wao huo umerejesha morali kwa wachezaji kufanya vizuri katika michezo ijayo.

Maria aliliambia Mwanaspoti, morali imerudi baada ya kupoteza mechi ya kwanza  dhidi ya Tausi Royals kwa pointi 58-55.

“Tuliumia sana baada ya kupoteza dhidi ya Tausi Royals kutokana na tulivyokamata mechi siku hiyo, kwani tuliongoza katika robo mbili za kwanza, kwa pointi 13-12 na 15-8.

Kisha wapinzani wetu wakaongoza robo ya tatu kwa pointi 16-12 na ya nne 22-15, kwa kweli tuliumia sana,” alisema Maria.

Akizungumzia ushindani  wa ligi hiyo upande wa wanawake 2026, amesema ni mkubwa tofauti na miaka iliyopita, ikichagizwa na bonasi zinazotolewa kwa kila mchezaji kwa timu itakayoshinda.

Kwa pande wa timu yake, amesema wamejipanga kuhakikisha wanashinda kila mechi kwa timu watakayokutana nayo mbele yao.

Kiongozi wa timu hiyo, Emanuel Mkono alisema mikakati waliyoiweka ni kuhakikisha inafanya vizuri WBDL mwaka huu.

Alisema alipata wazo la kuanzisha timu mwaka jana baada ya kuona za wanawake hazipati sapoti kubwa kwa wadau wa mchezo.

“Kwa uwezo wangu niliona niwape sapoti na kuwapa thamani kwenye mchezo huu,” alisema Mkono.