Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Azam yamsaka kiungo wa Power Dynamos

Muktasari:

MATAJIRI wa Ligi Kuu Bara, Azam FC wanaendeleza kuimarisha kikosi chao kwa kuwaongezea mikataba baadhi ya wachezaji muhimu ambao inamalizika pamoja na kuingia sokoni kuangalia wale wapya ambao wanaweza kuziba mapungufu ya msimu huu.

MATAJIRI wa Ligi Kuu Bara, Azam FC wanaendeleza kuimarisha kikosi chao kwa kuwaongezea mikataba baadhi ya wachezaji muhimu ambao inamalizika pamoja na kuingia sokoni kuangalia wale wapya ambao wanaweza kuziba mapungufu ya msimu huu.

Azam FC, katika kuingia kwao sokoni wamenasa kwa kiungo wa Power Dynamos, Benson Sakala inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Zambia.

Kama mambo yatakwenda vizuri juu ya kiungo huyo halitakuwa jambo la kushangaza kwake kumuona akiwa katika viunga vya Azam Complex akiipigania timu hiyo.

Kama Azam watafanikiwa kumsajili Sakala au mchezaji mwengine wa kigeni katika dirisha kubwa la usajili ambalo linakuja maana yake watalazimika kupunguza mchezaji mmoja wa kigeni waliokuwa nao wakati huu.

Katika kikosi cha Azam FC, tayari kuna wachezaji kumi kama ambavyo sheria za ligi zinavyohitaji.

Wachezaji wa kigeni waliokuwa katika kikosi cha Azam Fc, Mathias Kigonya, Bruce Kangwa, Nicolas Wadada, Daniel Amoah, Yakub Mohammed, Prince Dube, Obrey Chirwa, Niver Tigere, Mpiana Monzinzi na Ally Niyonzima.

Kutokana na viwango ambavyo vimeonyeshwa na wachezaji wa kigeni wa Azam Fc, msimu huu kuna wachezaji watatu ambao halitakuwa jambo la kushangazwa kama wakionyeshwa mlango wa kutokea.

Katika hatua nyingine uongozi wa Azam FC, umevunja ndoto na mawazo ya mashabiki na wapenzi wa soka kutokea Simba na Yanga juu ya kinara wa mabao, Dube kwenda katika moja ya timu hizo kongwe nchini hapo msimu ujao.

Ndoto hizo zimefutwa baada ya Azam Fc, kumuongeza mkataba wa miaka miwili Dube ambao utamalizika mwisho wa msimu wa 2023-24.