AS Vita yavunja rekodi ya Simba

New Content Item (1)
New Content Item (1)

BAADA ya Simba kutamba kwa muda mrefu na rekodi ya kutoruhusu bao katika hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika hatimaye, AS Vita imeivunja rekodi hiyo.

Hilo limejiri kwenye mchezo wa mkondo wa pili wa hatua ya makundi unaoendelea katika dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Mchezo huo ulioanza saa 10:00 jioni ulikuwa na ushindanoi wa aina yake kutokana na timu zote kuanza kwa mashambulizi ya kasi na kosa kosa za hapa na pale.

Dakika ya 30, Luis Miquissone akaitanguliza Simba kwa shuti kali baada ya kupokea mpira kutoka kwa Bernard Morisson aliyefanya kazi kubwa ya kuwatoka mabeki na kuingiza mpira ndani ya boksi.

Bao hilo halikudumu sana kwani dakika ya 32, kiungo wa AS Vita, Zemanga Soze alisawazisha kwa shuti kali na kuvunja rekodi ya Simba ambayo haikuwahi kuruhusu bao katika hatua hiyo ya makundi.

Hata hivyo mwamba wa Lusaka, Clatous Chama aliweka kambani bao la pili katika dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza na kuipeleka Simba mapumziko ikiwa kifua mbele.