Arsenal yakataa ofa kumuuza Lacazette

Wednesday September 30 2020
chelsea pic

 LONDON, ENGLAND. ARSENAL imeripotiwa kukataa ofa ya AS Roma kuhusu kumnasa straika Alexandre Lacazette.

Miamba hiyo ya Emirates bado inataka kuboresha kikosi chao dirisha hili kabla halijafungwa, wakifukuzia huduma ya viungo wa Lyon, Houssem Aouar na Thomas Partey wa Atletico Madrid.

Lakini, Arsenal kupata pesa za kunasa huduma za wachezaji hao itabidi isajili kwake. Kwa mujibu wa The Athletic, Roma wanahitaji sana saini ya Lacazette, lakini pesa waliyoweka kwenye meza ya Arsenal kutaka kumnasa mchezaji huyo haitoshi na wamesisitiza hawana mpango wa kuongeza.

Lacazette bado hajaanza mazungumzo yoyote kuhusu mkataba mpya na jambo hilo linawapa wasiwasi huenda anataka kuondoka. Mkataba wake wa sasa utafika tamati Juni 2022.

 

Advertisement