Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal wakichangamka wanambeba Hakim Ziyech

Muktasari:

  • Ziyech amebakiza mkataba wa miaka miwili kwenye kikosi hicho na bei yake anayouzwa ndio hiyo Pauni 25 milioni ikiwa ni zaidi ya nusu ya bajeti nzima ya usajili ya kocha Unai Emery kwenye dirisha hili ambayo ni Pauni 40 milioni.

LONDON, ENGLAND.ARSENAL wamepata matumaini mapya ya kumnasa staa wa Ajax, Hakim Ziyech baada ya winga huyo mwenyewe kuwa tayari kwenda kukipiga Emirates.
Mwandishi wa mambo ya soka wa Uholanzi, Marcel van der Kraan alisema staa huyo wa kimataifa wa Morocco yupo tayari kuachana na Ajax kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi na kwenda kukipiga kwenye Ligi Kuu England.
Ziyech alikuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Ajax chini ya kocha Erik ten Hag ambacho kilibeba ubingwa wa Eredivisie na kukomea nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakisukumwa nje na Tottenham msimu uliopita. Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Ajax, Marc Overmars, alisema Ziyech, ambaye mkataba wake kuna kipengele kinachohitaji kulipwa Pauni 25 milioni kwa timu inayotaka kumsajili, yupo huru kuondoka mwaka huu.
Winga huyo alitua kwenye kikosi cha Ajax miaka mitatu iliyopita akitokea FC Twente, amefunga mabao 21 na kuasisti mara 18 kwenye mechi zote alizocheza msimu uliopita.
Ziyech amebakiza mkataba wa miaka miwili kwenye kikosi hicho na bei yake anayouzwa ndio hiyo Pauni 25 milioni ikiwa ni zaidi ya nusu ya bajeti nzima ya usajili ya kocha Unai Emery kwenye dirisha hili ambayo ni Pauni 40 milioni.
Van der Kraan alisema: "Nafahamu mchezaji huyo yupo tayari kwenda kujiunga na timu kama Arsenal, ambayo siku zote inachez mpira mzuri. Manchester City chini ya Pep Guardiola pia wanacheza staili ya Ajax sawa na ilivyo kwa Barcelona. Lakini si kwamba klabu hizo zote zinamtaka. Nadhani kama Arsenal watamchoka Mesut Ozil, huyu Ziyech anaweza kuwafaa."