Aliyemvaa Chama, kuongoza msafara Ahly

Muktasari:

  • Hossam Ghaly ambaye amestaafu soka mwaka 2018, amewahi kukabana na kiungo wa Simba  Clatous Chama mwaka 2011 kwenye mchezo wa kwanza wa raundi za awali kule Zambia dhidi ya Zesco ambao ulimalizika kwa suluhu.

Zikiwa zimebakia siku kadhaa kabla ya mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba na Al Ahly Misri, ambao mabosi wa timu hiyo wamemteua kiungo wa zamani Hossam Ghaly aliye Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi kwa sasa kuongoza msafara unaokuja jijini Dar es Salaam.


Hossam Ghaly ambaye amestaafu soka mwaka 2018, amewahi kukabana na kiungo wa Simba  Clatous Chama mwaka 2016 kwenye mchezo wa hatua ya  makundi uliopigwa  kule Zambia dhidi ya Zesco ambao ulimalizika kwa Zesco kushinda  mabao 3-2,.


Kwenye mechi hiyo, Ghaly aliyekuwa akitumika kama kiungo mkabaji alicheza kwa dakika zote 90, lakini Chama alifanikiwa kufunga mabao mawii.
Fundi huyu ambaye hadi anastaafu alishinda mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa akiwa na Ahly, atasaidiwa na meneja wa timu hiyo, Khaled Bibo katika suala la kuongoza msafara na kufanya maandalizi ya wababe hao hapa nchini.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ahly, kazi ya wawili hawa ni kuhakikisha wanapanga jinsi timu itakavyosafiri kutoka Misri hadi Tanzania, kuanzia ishu za hoteli, chakula na mahali ambako watakuwa wanafanyia mazoezi.


Simba inatarajia kukutana na Ahly, Ijumaa ya Machi  29 kuanzia saa 3:00 usiku kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kabkla ya kurudiana wiki moja baadae mjini Cairo, Misri.


Hii ni mara ya nne kwa timu hizo kukutana katika michuano ya CAF, lakini ni mara ya kwanza kwa hatua ya robo fainali.


Mara zilishakutana katika mechi za makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kila moja kushinda mchezo wa nyumbani, huku mwishoni mwa mwaka jana zilikutana tena katika michuano mipya ya Ligi ya Afrika (African Football League) na kushindwa kutambiana kwa kutoka sare ya 2-2 jijii Dar na 1-1 Cairo Misri na Al Ahly kutinga nusu fainali kwa faida ya kanuni ya bao la ugenini.