Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

AFCON 2027: Wizara ya Maliasili na Utalii kuzipa hadhi hoteli  za kitalii  

UTALII Pict

Muktasari:

  • Zoezi hilo litahusisha ukaguzi wa kina wa miundombinu, usafi, ubora wa chakula, pamoja na huduma kwa wateja ili kuhakikisha zinakidhi viwango vya kimataifa.

IDARA ya Utalii kwa kushirikiana na Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara ya Maliasili na Utalii, imesema inatarajia kuanza mchakato wa kupanga hadhi (Grading and regrading) kwa watoa huduma wa hoteli na chakula nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Mei Mosi, 2026, na Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Dk Thereza Mugobi, mchakato huo ambao ni wa kawaida ni hatua muhimu ya kujiandaa na ongezeko kubwa la wageni linalotarajiwa kuingia na kuhudumiwa nchini wakati wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika  (AFCON 2027)

Pia amesema unalenga kuinua ubora wa huduma ili kuiwezesha Tanzania kujitangaza kimataifa kama kitovu cha utalii na ukarimu barani Afrika huku akidokeza kuwa zoezi hilo litaanza mwanzoni mwa mwezi Mei hadi Juni 2026 katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Kilimanjaro.

Zoezi hilo litahusisha ukaguzi wa kina wa miundombinu, usafi, ubora wa chakula, pamoja na huduma kwa wateja ili kuhakikisha zinakidhi viwango vya kimataifa.

Amewataka wamiliki na watoa huduma wa hoteli kutumia fursa hiyo kujipima kiwango cha ubora wa huduma huduma wanazotoa ili kuvutia na kuwahifadhi wageni kabla, wakati na baada ya AFCON 2027.

Kupitia zoezi hilo la hadhi ya nyota kwa hoteli itatolewa huku likizingatia ubora ambapo zilizokidhi zitapandishwa na zile zisizokidhi zitashushwa.