
Dar es Salaam.Timu ya Taifa ya Tanzania chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) itacheza mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Morocco Machi 17, 2018 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo huo ni wa kujiandaa na mchezo wa kuitafuta tiketi ya kucheza fainali za Afrika kwa Vijana dhidi ya DR Congo utakaochezswa Machi 31, 2018.
Morocco wanatarajia kutua nchini Machi 14,2018 ikiwa na msafara wa watu 31 wanaojumuisha wachezaji 23 na viongozi 8 wa benchi la ufundi.
Tayari kocha Kim Poulsen amewaita kambini wachezaji 40 wa Ngorongoro Heroes, kujiandaa na mchezo wa raundi ya kwanza ya kuitafuta tiketi ya kucheza fainali za vijana za Afrika dhidi ya DR Congo mchezo utakaochezwa Machi 31, 2018 kwenye Uwanja wa Taifa.
Kikosi kilichoingia kambini makao Makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Machi 6, 2018 ni wachezaji 40 ambao watapunguzwa na kubaki wachezaji 30 baada ya kumalizika wiki ya kwanza ya mazoezi.
Kikosi kilichoingia kambini: Ramadhan Kabwili(Yanga), Abutwarib Mshedi (Mtibwa), Johny Kwiyenda(Makongo), Ally Salim (Simba), Kibwana Shomari (Mtibwa), Ally Msengi (Mbao), Enrick Nkosi(African Lyon), Dikson Job(Mtibwa), Assad Juma(Singida United).
Pia wapo Said Bakary (Yanga), Ally Ng’anzi(Singida United), Kelvin Naftal (JKT Tanzania), Shaban Ada(Lipuli), Issa Makamba (Singida United), Mohamed Rashid (Singida United),Marko Gerald(JMK), Syprian Mtesigwa (Dodoma FC), Muhsin Makame(Njombe Mji).
Yohana Mkomola(Yanga), Ibrahim Abdallah (Miembeni City), Abdul Suleiman (Ndanda), Nickson Kibabage(Njombe Mji), Mussa Najimu(Changanyikeni), Maziku Aman(Makongo)
Wengine ni Hamis Mustafa(Ndanda), Samson Myati (Toto Africans), Said Mohamed(Azam FC), Ayoub Mohamed(Yanga), Mohamed Mussa(Azam FC), Emanuel Myati(Tz Prisons), Riffat Hamis (Mtibwa), Oscar Masai(Azam FC).
Paul Peter (Azam FC),Vitalis Mayanga (African Lyon), Rajab Mohamed(Azam FC), Pontia Ohonya, Maka Anthony(Yanga), Israel Mwenda (Alliance), Hance Msonga (Alliance) na Moses Kitandu(Simba)