Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mayele kutetema Zenji leo

Mayele kutetema Zenji leo

BAADA ya kutwaa mataji, kiungo fundi wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amemvusha maji Fiston Mayele tayari kwaajili ya mchezo wa kirafiki wa kuchangia watoto wenye uhitaji kisiwani Unguja.

Mchezo huo maalum utakaochezwa leo Jumatano, kwenye Uwanja wa Amaan, utazikutanisha Team Road na Magari ya Mchanga.

Akizungumza na Mwanaspoti, Fei Toto alitaja mastaa atakaosafiri mbali na Mayele kuwa ni Ibrahim Abdallah ‘Bacca’, Abubakar Salum ‘Sure Boy’ na kiungo wa KMC, Awesu Awesu huku akiweka wazi mastaa wengine watakuwa sapraizi kwa watazamaji.

Alisema wanaamua kurudisha kidogo wanachokipata kwa jamii inayowazunguka wanaamini kidogo kitakachopatikana kinaweza kutatua shida za watoto wenye uhitaji.

“Nipo upande wa Team Road na timu yangu mshambuliaji ni Mayele hii ni ya wachezaji wote wa Zanzibar wanaocheza Bara na Visiwani tunatarajia mchezo mzuri,” alisema na kuongeza;

“Nacheza nje na nyumbani kwetu wanaamini nina kitu kikubwa nakipata siwezi kuwasaidia kwa namna moja au nyingine kwa kile kidogo ninachokipata ndio maana nimeamua kufanya hicho kitakachofanyika Jumatano,” alisema.

Fei Toto alitumia nafasi hiyo kuwaomba wazanzibari kujitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo huo ili kuchangia chochote kwa watoto wenye uhitaji wakija kushuhudia mastaa.