Man United wapo siriazi kwa De Ligt
Muktasari:
Kinachoelezwa ni kwamba Man United kwa sasa wanasubiri tu Ajax wawajibu na kuwaita kwa ajili ya mazungumzo baada ya yale yaliyokuwa yakizungumza kuhusu beki huyo kwenda Juventus kudaiwa kukwama.
MANCHESTER, ENGLAND.MANCHESTER United wanaripotiwa kwamba bado hawajafuta mpango wao wa kumsajili beki wa kati wa Ajax, Matthijs de Ligt.
Kinachosemwa ni kwamba Man United wameshapeleka ofa yao ya kumnasa beki huyo wa Kidachi na kwamba kila kitu kipo mezani kwa Ajax.
Mwandishi wa masuala ya usajili wa BBC Sport, David Ornstein alisema kwamba Man United ni klabu ya kwanza na pekee iliyopeleka ofa rasmi ya kutaka huduma ya De Ligt baada ya kukoshwa na kiwango chake cha msimu uliopita.
Kinachoelezwa ni kwamba Man United kwa sasa wanasubiri tu Ajax wawajibu na kuwaita kwa ajili ya mazungumzo baada ya yale yaliyokuwa yakizungumza kuhusu beki huyo kwenda Juventus kudaiwa kukwama.
"Hivi karibuni niliambiwa kwamba ofa pekee ya kuhusu (Matthijs) De Ligt iliyopo mezani, ambayo sio ya maneno maneno na ambayo inaweza kutiki ni ya kutoka Manchester United," alisewma Ornstein kupitia posti yake kwenye mtandao wa kijamii.
“Utakuwa ni uamuzi wa mchezaji kwamba kukataa kwenda kujiunga na timu hiyo."