Kipigo cha 5-1 Dar chawaamsha Platinum
KIPA wa FC Platinum ambaye pia ni nahodha, Petros Mhari amesisitiza kwamba kamwe hawawezi kurudia makosa kama ya kipindi cha pili waliyofanya dhidi ya Yanga mwaka 2015 kwenye meci ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Katika msimu huo ambao FC Platinum walitolewa na Yanga walishindwa kumudu mchezo kipindi cha pili kutoka na hali ya hewa ya joto ambayo walikuwa hawajaizoea kwa kuchelewa kuwasili Dar es Salaam. Yanga ilishinda mabao 5-1 nyumbani na kufungwa bao 1-0 ugenini.
Kipa huyo amesisitiza jana kwamba wamejifunza kutokana na kosa hilo na halitajirudia kwenye mechi na Simba kesho.
“Tumeambiwa mpaka mazoezini kwamba tunapaswa kupambana mwanzo mwisho vipindi vyote viwili ili tusirudie yale makosa yaliyotutoa,” alisema. Simba inahitaji ushindi wa mabao 2-0 kusonga mbele kwenye hatua ya makundi ya michuano hiyo mikubwa Afrika.