Simba imetembelea Bunge la Tanzania, leo, Jumanne, Februari 4, 2025, siku mbili baada ya kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tabora United katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora.
Msafara wa Simba bungeni umeongozwa na wajumbe wa bodi ya wakurugenzi, Selemani Haroub na Issah Masoud.
Pia alikuwepo mtendaji mkuu wa klabu hiyo, Zubeda Sakuru, benchi la ufundi chini ya kocha Fadlu Davids na kikosi cha timu hiyo.