Klabu za Arsenal na Newcastle zimezidi kuwa na muendelezo mzuri wa matokeo katika Ligi Kuu England baada kushinda mechi za jana na kujihakikishi nafasi za juu kabisa kwenye msimamo wa ligi hiyo.
Newcastle iliifunga Chelsea bao 1-0 na kupanda hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 30 huku Arsenal ikiichapa Wolves mabao 2-0 na kujihakikishia nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 37, tano zaidi ya Man City inayoshika nafasi ya pili.